Spiritual Healing
Baada ya kujifungua, wanawake wanaweza kukumbwa na
matatizo mbalimbali.
Kwa kujikinga nayo kabisa, andika mchoro iliyotolewa
katika kitabu kwenye karatasi ya nta kwa rangi ya manjano na uitengeneze kuwa
hirizi.
Njia ya kutengeneza hirizi ni hii:
Chukua nyuzi kumi na moja (11) za uzi mbichi wa buluu
na zipime kwa urefu wa mwanamke.
Zikunje mara kadhaa mpaka baada ya kufungwa mafundo
kumi na moja (11) ziweze kuvaliwa shingoni kwa urahisi.
Kisha soma mara tatu:
يَا رَحِيمْ يَا اللّٰهُ يَا مُرِيدُ
Yaa Raheem, Yaa Allaah, Yaa Mureed
Pulizia na funga fundo moja.
Kwa namna hiyo tengeneza mafundo kumi na moja (11) kwa
nafasi zinazokaribiana.
Baada ya kuoga kwa ajili ya kumaliza kipindi cha baada
ya kujifungua, hirizi hii iondolewe shingoni na izikwe ardhini.