Topics
Kwa kawaida imeonekana kwamba watu wenye mishipa
dhaifu huwa na hasira nyingi. Wakati mwingine pia mtu huwa mkali kutokana na
mazingira magumu, hisia za kunyimwa haki, au kujiona bora kuliko wengine.
Pia imeonekana kwamba baadhi ya watu ambao nje ya
nyumba huwa watulivu na wenye subira, lakini wanapokuwa mbele ya wake na watoto
wao huwa wakali. Mara nyingi ndani yao huwa na hamu ya kutawala wengine.
Ikiwa mgonjwa mwenyewe anataka kuondokana na hasira,
wakati wa hasira asome mara moja:
يَا وَدُودُ
Yā Wadūd
Kisha apulizie ndani ya maji na ayanywe kwa mafundo
matatu.
Ikiwa watu wa nyumbani wanataka kuondokana na hasira
za mtu mmoja au zaidi, kabla ya kuchomoza jua wasome mara moja:
يَا وَدُودُ
Yā Wadūd
juu ya funda moja la maji na wamnyweshe akiwa bado
hajala chochote.
Ikiwa hilo haliwezekani, maji yaliyosomewa yawekwe
ndani ya mtungi au chombo cha maji kinachotumiwa na watu wote wa nyumbani.
Muda wa kufanya Matendo ya Kiroho hii ni hadi siku
arobaini (40).